Simba kicheko Katiba mpya

Simba kicheko Katiba mpya

Na Mwandishi Wetu 

SERIKALI kupitia ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo na Vilabu imeidhinisha na kuikabidhi rasmi klabu ya Simba katiba yao mpya huu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Paul Makonda alilolitoa Februari 16,2026.

Akizungumza  Februari 18, 2026,  Msajili wa Vyama vya Michezo na Vilabu Wakili Abel Ngilangwa amenukuliwa akisema “kupitia maelekezo ya Waziri Ofisi ya Msajili imeshakamilisha hatua hiyo ya mwisho ya kukabidhi Katiba na kupokelewa rasmi kwahiyo katiba ya Simba imeshakabidhiwa kwenye Uongozi wa klabu ya Simba”

“Kwa msingi huo napenda Februari 18,2026 kuutarifu umma kuwa mchakato wa marekebisho ya katiba ya Simba SC. sasa umehitimishwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria na kanuni ya Vyama vya michezo baada ya kukamilika kwa hatua zote ikiwemo kukabidhi rasmi katiba hii kwa klabu ya Simba”

“Mchakato huu wa marekebisho ya katiba ya Simba umepitia michakato mingi kuanzia uchambuzi, tathmini na uidhinishaji wa marekebisho ya katiba, yote haya yalikuwa yameshafanyika ulibakia mchakato mmoja wa kuwakabidhi Simba katiba yao maana walishawasilisha katiba tukawa tunawasiliana nao kupata ufafanuzi tofautitofauti ili katiba ibebe madhumuni yaliyokusudiwa, mchakato wa mwisho ni kukabidhi katiba na wakati wa kukabidhi Uongozi wa Simba unasaini kuthibitisha unakubali kuwa haya marekebisho sahihi na yamebeba maudhui yaliyotakiwa ambapo tayari hatua hiyo ya kukabidhi imefanyika”

You may also like

Ulaji vyakula vya viwandani chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza

Ulaji vyakula vya viwandan...

Simba kicheko Katiba mpya

Simba kicheko Katiba mpya

Maneno afichua siri Kliniki ya bure

Maneno afichua siri Kliniki...

GAZETI LA WATANZANIA 19/02/2026

GAZETI LA WATANZANIA 19/02/...